preloader

Kila taarifa na habari kuhusiana na jukwaa la panda digital zinapatikana hapa.

Panda Chat
  • Habari:UZINDUZI WA ONGEA HUB SMS
  • Muda:2024-03-13 15:39:09

Taasisi Ya Her Initiative Inayo Endesha Jukwaa Kubwa La Panda Digital Imezindua Jukwaa Jipya La Ongea Hub Upande Wa Jumbe Za Simu (SMS). Panda Digital Ni Ni Jukwaa La Kidigitali La Kwanza La Kiswahili Lenye Lengo La Kuwasaidia Wasichana Kupata Ujuzi Na Rasilimali Za Kuanza Na Kuendesha Biashara Zao Ili Kufikia Uchumi Wa Kidigitali. ONGEA Hub Ni Jukwaa La Kiswahili La Kidigitali Ndani Ya Panda Digital Linalowapa Nafasi Wasichana Wajasiriamali  Kuripoti Kesi Za Rushwa Ya Ngono Na Kuwaunganisha Na Mamlaka Zinazotoa Msaada Wa Kisheria, Kisaikolojia, Kijamii Na Kihisia. 

Tatizo La Rushwa Ya Ngono Kwa Wasichana Wajasiriamali Limeendelea Kuwa Changamoto Kubwa Sana Tanzania. Japo Kuwa Hakuna Tafiti Za Moja Kwa Moja Zinazo Elezea Ukubwa Wa Tatizo Hili Kwa Wasichana Wajasiriamali, Lakini Yapo Makundi Ambayo Tafiti Zimebainisha Jinsi Rushwa Ya Ngono Imeathiri Makundi Hayo.

Ongea  Hub SMS Ni Suluhisho Kwa Wasichana Wajasiriamali Wanaopitia Adha Ya Rushwa Ya Ngono Lakini Hawamiliki Simu Janja Au Hawana Upatikanaji Mzuri Wa Mtandao, Pia Hawajui Msaada Gani Wanahitaji Au Wanaogopa Kuwashtaki Wahusika Wakihofia Sababu Tofauti Ikiwemo Woga Na Aibu Kutoka Kwa Jamii. 

 

Jukwaa Hili Lilianza Katika Mfumo Wa Tovuti, Ila Baada Ya Kugundua Kuwa Wapo Mabinti Pembezoni Mwa Miji Ambao Hawana Uwezo Wa Kutumia Tovuti Yetu Kutokana Na Sababu Kama Miundombinu Ya Kimtandao, Kutokuwa Na Simu Janja Na Pia Kushindwa Kumudu Huduma Za Intaneti . Kwa Sasa Jukwaa Hili Linapatikana Kwa Njia Ya SMS Ambapo Wasichana Wanapata Nafasi Kuelezea Kesi Zao Na Kisha Kuorodhesha Aina Ya Msaada Wanaohisi Utawasaidia Zaidi. Hii Inawawezesha Kuwaweka Karibu Na Mashirika Na Taasisi Zinanzofanyia Kazi Changamoto Ya Rushwa Ya Ngono. Her Initiative Inajitolea Kuhakikisha Kuwa Mabinti Wanapata Msaada Unaofaa Kutoka Kwa Wadau Mbalimbali Ikiwemo PCCB, Madawati Ya Jinsia, Wataalamu Wa Saikolojia Na Wadau Wa Haki Za Binadamu.

 

Akizungumzia Uzinduzi Huu Muhimu, Mkurugenzi Wa Her Initiative, Bi. Lydia Charles Moyo Alisema, "Ongea Hub Inatumia Fursa Iliyopo Katika Majukwaa Ya Kidigitali Kufikia Wasichana Wengi Zaidi Na Kurahisisha Ufikiwaji Wa Msaada Kwa Njia Salama Bila Hofu Ya Kuhukumiwa”. Anaendelea Kusema Kupitia ONGEA Hub Wasichana Wanaweza Kuripoti Katika Lugha Ya Kiswahili Na Bure Bila Malipo Yoyote.

Jukwaa Hili Ni Muhimu Kwa Wasichana Kama Mimi, Kwasababu Linatupa Nafasi Ya Kuweza Kupaza Sauti Zetu Na Kuwa Huru Katika Kubainisha Matukio Ya Ukatili Kama Rushwa Ya Ngono, Ndio Maana Likaitwa ONGEA Hub Kwa Kumaanisha Ni Wakati Wetu Sasa Kuvunja Ukimya Juu Ya Rushwa Ya Ngono; Msichana Kinara Wa Kupinga Rushwa Ya Ngono. 

Ili Kutumia Jukwaa Hili, Tuma Neno SAJILI Kwenda Namba 0767 680 463 Na Kwa Wale Wanaomiliki Simu Janja Wanaweza Tembelea Tovuti Yetu Www.pandadigital.co.tz Na Chagua ONGEA HUB Kwenye Menyu Kuu. Hapo Utapata Fomu Itakayokuhitaji Ujaze Taarifa Zako. Ni Muhimu Kuzingatia Kuwa Mfumo Wa Uwasilishaji Wa Jukwaa Hili Ni Wa Siri Kabisa Na Unaheshimu Na Kulinda Taarifa Za Msichana. 

 

UZINDUZI WA ONGEA HUB SMS

Habari Nyingine