UNLOCK THE POTENTIAL OF YOUR SOCIAL BUSINESS WITH US
The Young Social Entrepreneurs (YSE) Global ni programu ya miezi minane inayohamasisha, kuandaa na kuwezesha vijana wa mataifa mbalimbali kuanzisha […]
Jukwaa la kwanza la kidigitali kwa lugha ya kiswahili lenye lengo la kuwasaidia wasichana kupata ujuzi na rasilimali za kuanza na kuendesha biashara zao ili kufikia uchumi wa kidigitali. Jukwaa hili linafahamika kama Panda Digital likiwa na maana yakupanda mbegu yakujitegemea kiuchumi kwa kutumia majukwaa ya kidigitali.
Hii ni njia itayowakusanya wasichana wote wajasiriamali na kuwapa nafasi ya kuchagua fursa mbalimbali zitazoendana na mahitaji yao kama vile ufadhili, fursa na mafunzo.
Jukwaa hili linatumia mfumo mseto wa uwasilishaji ili kunufaisha wasichana wa makundi tofauti mijini na vijijini. Mfumo wa kwanza ni Panda website/tovuti ambapo msichana anaweza kunifaika kwa kutembelea tovuti yetu ya https://pandadigital.co.tz/
Mfumo wa pili ni kupitia PANDA SMS ambalo ni jukwaa la kiswahili la kidigitali mahususi kwa ajili ya wasichana kupata ujuzi wa kuanza na kuendesha biashara zao kupitia SMS za kawaida. Ukitumia PANDA SMS huna haja ya kuwa na data kusoma kozi na kuona fursa. TUMA neon SAJILI kwenda namba 0767680463 kuanza kujifunza.
Panda tovuti na PANDA SMS ni majukwaa kwaajili wasichana kupata ujuzi wa dijiti ili kuwasaidia wakuze biashara zao. Kumbuka Maudhui haya hutolewa bure kabisa na unatunukiwa cheti kila umalizapo kozi.
Soko Mtandao ni miongoni mwa eneo la kimasoko linalokua zaidi si tu Tanzania, bali duniani kote. Vilevile, katika ulimwengu wa sasa, huduma nyingi zinatolewa katika namna ambayo ni rahisi zaidi kwa mtoaji na mpokeaji.
Kwa mjasiriamali, basi kuna kundi kubwa la wateja ambao kabla hawajafikia uamuzi wa kufanya manunuzi watatafuta taarifa na kufuatilia maelezo ya bidhaa na biashara hizo kupitia mtandao.
Vilevile, soko mtandao limethibitika kuwa muhimu katika nyakati zenye mashaka kama vile nyakati za janga la corona, na kusaidia uendelevu wa biashara hata katika wakati ambao wateja hawawezi kufika katika eneo biashara inapopatikana.
Kiukweli nimejifunza mengi sana maana kuna vitu hata nilikuwa sijui kuwa sijui..
Hatimaye kusoma mtandaoni kwa lugha ya kiswahili, kiukweli ni jambo kubwa sana.
Unajua haya masuala sijui ya kidigitali tulidhani hayatuhusu kabisa yaani..
Saa zingine unahitaji mtu wa kukushika mkono na kukupa ujuzi. Kwangu ni Panda.
Mtandao wa Panda umetengenezwa kwa kuwezeshwa na taasisi hizi.
Pata taarifa mbalimbali kuhusu fursa ndani ya mtandao Panda pamoja na matukio tunayoyafanya kwa ground.
The Young Social Entrepreneurs (YSE) Global ni programu ya miezi minane inayohamasisha, kuandaa na kuwezesha vijana wa mataifa mbalimbali kuanzisha […]
Program ya miaka 10, inayolenga kutumia dola milioni 100 kutambua, kutoa mafunzo, kushauri na kufadhili wajasiriamali 10,000 wa Kiafrika. Lengo […]