Jifunze zaidi kuhusu Panda Digital na jinsi tunavyowasaidia wasichana kunufaika uchumi wa kidigitali
Jukwaa la kwanza la kidigitali kwa lugha ya Kiswahili lenye lengo la kuwasaidia wasichana kupata ujuzi na rasilimali za kuanza na kuendesha biashara zao ili kunufaika uchumi wa kidigitali. Jukwaa hili linafahamika kama Panda Digital likiwa na maana ya kupanda mbegu ya kujitegemea kiuchumi kwa kutumia majukwaa ya kidigitali.
Hii ni njia inayowakusanya wasichana wote wajasiriamali na kuwapa nafasi ya kuchagua fursa mbalimbali zinazoendana na mahitaji yao kama vile ufadhili, fursa na mafunzo. Jukwaa hili linatumia mfumo mseto wa uwasilishaji ili kunufaisha wasichana wa makundi tofauti mijini na vijijini.
Kuwa jukwaa la kwanza la kidigitali kwa lugha ya Kiswahili lenye lengo la kuwasaidia wasichana kupata ujuzi na rasilimali za kuanza na kuendesha biashara zao ili kunufaika uchumi wa kidigitali.
Kuwa na jamii ya wasichana wajasiriamali wenye ujuzi wa kidigitali na uwezo wa kujitegemea kiuchumi kupitia teknolojia na majukwaa ya kidigitali.
Thamani zinazotufanya kuwa tofauti na kuwa na imani yetu
Tunaamini katika umoja na ushirikiano wa wasichana wote
Tunaamini katika nguvu ya elimu na ujuzi wa kidigitali
Tunaamini katika uaminifu na uwazi katika kila kitu tunachofanya
Tunaamini katika kuwawezesha wasichana kuwa na uwezo wa kujitegemea
Unakaribishwa kujiunga na jukwaa letu na kuanza safari yako ya kujitegemea kiuchumi kupitia teknolojia ya kidigitali.