preloader

Kila taarifa na habari kuhusiana na jukwaa la panda digital zinapatikana hapa.

Panda Chat
  • Mnufaika:Halima Msofe
  • Muda:2024-03-13 11:42:28
  • Kuhusu:Kuwawezesha Wasichana Kupambana Na Rushwa Ya Ngono

Halima Msofe, Mwanafunzi Mwenye Azma Katika Chuo Kikuu Cha Dodoma, Alisimama Kama Kinara Dhidi Ya Rushwa Ya Ngono Katika Kampeni Za Mwaka 2022. Alitambua Haja Kubwa Ya Kushughulikia Suala Hili. Mienendo Ya Kijamii Iliyopo Ililazimisha Kimya Kilichokuwa Kinaogofya Kuzunguka Suala Hili.

Wakati Her Initiative Ilipoposti Kwenye Instagram, Wakitafutavinara Watakao Ongoza Kampeni Ya Kupinga Rushwa Ya Ngono, Halima Alitumia Fursa Hiyo Kutoa Sauti Yake Kwa Sababu Hiyo.

Kushiriki Katika Kampeni Hii Ya Panda Movement Ilimbadilisha Sana Na Kumtengeneza Kuwa Halima Mpya. Kupitia Kampeni Hii, Halima Alishuhudia Matokeo Chanya Yaliyoletwa Na Maamuzi Yake Ya Kuvunja Ukimya.

 

Juhudi Zake Zilihamasisha Na Kuwatia Moyo Wengine Kusimama Dhidi Yarushwa Ya Ngono. Aliwasiliana Na Kuwawezesha Wanawake Wasichana Wengine 30. Leo, Halima Anawahimiza Wenzake Kujiunga Na Mapambano Dhidi Ya Ukatili Wa Kijinsia Haswa Rushwa Ya Ngono, Akisisitiza Kuwa Ni Hatua Muhimu Kwenye Njia Yao Ya Mafanikio.

 

Kuwawezesha Wasichana Kupambana Na Rushwa Ya Ngono

Wanufaika Wengine