preloader

Katika eneo hili tunakuletea taarifa za fursa mbalimbali kama vile elimu bora, upatikanaji wa rasilimali, na mazingira yanayowezesha kujifunza na kukuza ujuzi.

fursa
  • Post:Pata Hadi Dola 15,000 Za Kimarekani Kwa Mjasiriamali Mpya Kupitia Programu Ya Mastercard Foundation FAST 2025"
  • Date:2025-04-17 14:12:33

Pata Hadi Dola 15,000 Za Kimarekani Kwa Mjasiriamali Mpya Kupitia Programu Ya Mastercard Foundation FAST 2025"

Je, Wewe Ni Kijana Mbunifu Unayetafuta Njia Ya Kuanzisha Au Kukuza Biashara Yako? Mastercard Foundation, Kwa Kushirikiana Na Mashirika Yanayoongoza Katika Maendeleo Ya Biashara Na Ubunifu Barani Afrika, Imezindua Rasmi Duru Ya Pili Ya Maombi Kwa Programu Ya FAST (Fund For Alumni Start-ups In Transition).

Hii Si Tu Fursa Ya Kupata Ufadhili, Bali Ni Jukwaa Lenye Mchango Mkubwa Katika Kukuza Uwezo Wa Ujasiriamali, Kukuunganisha Na Wataalamu, Pamoja Na Kujenga Na Kuendeleza Mtandao Wa Ushirikiano Ndani Ya Afrika.

Faida Na Fursa Zinazotolewa Na Programu

1. Ufadhili Wa Hadi Dola 15,000 Za Kimarekani Kwa Kila Mradi Utakaochaguliwa
Fedha Hizi Zinatolewa Kulingana Na Kiwango Cha Maendeleo Ya Biashara Yako

  • Hatua Ya Kukuza Wazo La Biashara: Takriban Dola 5,000 Za Kimarekani Kusaidia Kuboresha Na Kuendeleza Wazo La Biashara
     
  • Hatua Ya Ujenzi Wa Biashara: Kati Ya Dola10,000 – 15,000 Za Kimarekani Kusaidia Kuanzisha Na Kukuza Biashara Yako Iwe Imara Na Endelevu
     

2. Mafunzo Ya Kukuza Biashara Yako
3.  Mshauri Binafsi (mentor) Kutoka Kwa Wataalamu Waliobobea
4.  Fursa Ya Kushirikiana Na Vijana Wengine Wabunifu Kutoka Afrika
5.  Fursa Ya Kuonekana Na Kutambulika Kupitia Mtandao Mpana Wa Mastercard Foundation

Sifa Za Mwombaji

Programu Hii Inalenga Wahitimu Kutoka Mitandao/programu Zifuatazo:

  • Young African Leaders Initiative (YALI)
     
  • African Leadership Academy (ALA)
     
  • Anzisha Prize
     
  • Mastercard Foundation Scholars Program
     

Ikiwa Unakidhi Mojawapo Ya Sifa Hizi:

  • Mjasiriamali Aliyeanzisha Biashara Changa.
     
  • Kijana Mwenye Wazo La Biashara Lenye Mwelekeo.
     
  • Unatafuta Mafunzo, Ufadhili Na Mtandao Wa Usaidizi.

Hii Ni Fursa Adhimu Ya Kusonga Mbele Katika Safari Yako Ya Ujasiriamali.

 

TAREHE ZA MUHIMU

  • Ufunguzi Wa Dirisha La Maombi: Aprili 3, 2025
     

  • Kikao Cha Mtandaoni Cha Kutoa Taarifa: Aprili 8, 2025, Saa 5:00 Asubuhi (EST)
     

  • Mwisho Wa Kutuma Maombi: Aprili 27, 2025
     

  • Jisajili Kushiriki Kikao Hicho Kupitia Kiunganishi Hiki:
     

  • Bonyeza Hapa Kujiandikisha:  Https://asu.zoom.us/webinar/register/WN_54TY

 

 


 USIKOSE NAFASI HII YA KIPEKEE

Ikiwa Una Nia Thabiti Ya Kuleta Mabadiliko Kupitia Biashara, Programu Ya FAST Itakupa Msaada Wote Utakaohitajika Kufikia Malengo Yako.

Tuma Maombi Sasa.
Tembelea: https://opportunitiesforyouth.org/2025/04/15/apply-now-mastercard-foundation-fast-program-2025-up-to-15000-in-venture-support-for-early-stage-entrepreneurs/#google_vignette

Fursa Nyingine

Chat Bot Muulize Zuri