preloader

Katika eneo hili tunakuletea taarifa za fursa mbalimbali kama vile elimu bora, upatikanaji wa rasilimali, na mazingira yanayowezesha kujifunza na kukuza ujuzi.

fursa
  • Post:WITO KWA WASHAURI (MENTORS) WASICHANA KUJITOLEA KATIKA MPANGO WA SAFEHER 2023/2024.
  • Date:2023-10-31 08:50:14

WITO KWA WASHAURI (MENTORS) WASICHANA KUJITOLEA KATIKA MPANGO WA SAFEHER 2023/2024.

Je Wewe Ni Mtaalamu Wa Kike Mwenye Uzoefu Katika Utengenezaji Wa Programu, Muundo Wa Bidhaa Au Sayansi Ya Data Kwa Angalau Mwaka Mmoja? Je Unashauku Ya Kusaidia Wengine Na Unataka Kuleta Matokeo Chanya Katika Tasnia Ya Teknolojia? Kama Ndivyo Unakaribishwa Kujiunga Na Mpango Wa SafeHer Kama Mshauri (mentor).

Mpango Wa SafeHer Umejitolea Kuwasaidia Wanawake Wanapoingia Katika Tasnia Ya Teknolojia. Waandaaji Wanaamini Kuwa Ushauri (mentorship) Ni Zana Yenye Nguvu Katika Makuzi Na Mafanikio. Pia Wanatizamia Kupata Washauri (mentors) Ambao Wanaweza Kushirikisha Utambuzi Wao Na Kutoa Mwongozo Kwa Wanafunzi Wenye Shauku Ya Kukua Kwenye Sekta Ya Teknolojia.

Faida

  • Wataalamu Watapewa Cheti Mwishoni Mwa Kipindi Cha Mentorship

Stahiki

  • Mwombaji Lazima Awe Mwanamke
  • Mwombaji Anatakiwa Kuwa Na Angalau Mwaka Mmoja Wa Uzoefu Katika Tasnia Ya Utengenezaji Wa Programu (software Development), Muundo Wa Bidhaa (product Design) Au Sayansi Ya Data (Data Science).

Maombi

Chini Ni Maelezo Zaidi;

  • Muda: Novemba 2023 Hadi Machi 2024
  • Juhudi: Washauri Wanatarajiwa Kukutana Kwa Angalau Masaa 2 Kila Kipindi Katika Wiki
  • Ulinganisho: Washauri Watalinganishwa Kulingana Na Maeneo Yao Ya Masomo, Pamoja Na Maslahi Ya Kazi Na Uzoefu.

https://tinyurl.com/4axyr4rm

 

Fursa Nyingine